“ Pambana na Shetani kwa upanga wa imani ambao ni ukweli kwani ukweli ndiyo utakaokuweka huru. ”
Imani ni nia ya kujua kisichoweza kujulikana na hupeleka watu kwenye ukweli. Kuamini hupotosha, na ni nia ya kudharau kinachoweza kujulikana.
~ Enock Maregesi
Ukitaka kujua maana halisi ya maisha yako kuwa tayari kufanya vitu vikubwa vitakavyohitaji nguvu ya Mungu kuvikamilisha – na kudumu katika maisha hayo kwa kafara ya maombi.
Wanasayansi wanasema hakuna Mungu kwa sababu hawawezi kumwona wala kumgusa. Lakini nao hawana akili kwa sababu hawawezi kuiona wala kuigusa.
Usiingilie mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu. Kuingilia mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu ni dhambi. Dhambi hiyo itakuathiri. Hivyo, jali mambo yako – ya mwingine Mungu anayafanyia kazi – hadi utakapoitwa na Mungu kuingilia kati. Kuingilia kati mambo ya mtu mwingine kunaweza kuathiri mpango wa Mungu katika maisha yake. Hivyo, acha.