Classy Quote logo
  • Home
  • Categories
  • Authors
  • Topics
  • Who said

Maisha Quotes

Maisha quote from classy quote

Usiingilie mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu. Kuingilia mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu ni dhambi. Dhambi hiyo itakuathiri. Hivyo, jali mambo yako – ya mwingine Mungu anayafanyia kazi – hadi utakapoitwa na Mungu kuingilia kati. Kuingilia kati mambo ya mtu mwingine kunaweza kuathiri mpango wa Mungu katika maisha yake. Hivyo, acha.

~ Enock Maregesi

Enock Maregesi Dhambi God God S Plan Kibali Life Maisha Mpango Wa Mungu Mungu Permission Sin

Wewe kuingilia mambo ya John ni sawa na kusema, ‘Mungu umeshindwa hebu ngoja na mimi nijaribu; ngoja niingilie kati kukusaidia juu ya maisha ya John Doe.’ Hiyo ni dhambi. Tena ni dhambi kubwa. Unajifananisha na Mungu; kwamba Mungu wa John Doe ameshindwa kwa hiyo mungu wewe ndiye utakayemtatulia matatizo yake. Amri kuu ya kwanza ya Mungu inasema, ‘Usiwe na miungu mingine ila mimi.’ Kuingilia mambo ya John tayari umevunja amri ya kwanza ya Mungu kwa kujifanya Mungu. Mungu ana mpango na maisha ya John, na anatumia matatizo yake kumfikisha kwenye takdiri aliyompangia. Hivyo, wewe si Mungu, acha Mungu afanye kazi yake. Mungu akikuruhusu kuingilia kati, yaani John akiamua kwa hiari yake mwenyewe kukuomba msaada wa mawazo au ushauri, maana yake ni kwamba Mungu amekuchagua wewe kuwa sehemu ya mafanikio ya John Doe.

~ Enock Maregesi

Enock Maregesi Dhambi God Help Life Maisha Mpango Msaada Mungu Plan Sin

Kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa raha ni rahisi kuliko kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa shida, na utahitaji imani kuendelea kumwamini wakati wa dhiki. Vipindi vigumu katika maisha yetu hutokea kwa kila mmoja wetu. Kuamini ya kwamba Mungu ana makusudi ya lazima kukuondolea vikwazo katika maisha yako ni vigumu sana wakati mwingine, lakini imani ndicho kitu cha muhimu zaidi unachotakiwa kuwa nacho katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa. Amani ya Mungu, ambayo huzidi hekima na maarifa yote ya kibinadamu, ni kuliamini neno la Mungu kwamba ni la kweli. Bila imani hutaweza kumfurahisha Mungu. Imani ni ufunguo wa nguvu, uwezo na neema ambavyo Mungu ametupangia. Kwa ufupi, Mungu ni mkubwa kuliko wewe na matatizo yako.

~ Enock Maregesi

Enock Maregesi Ability Amani Ya Mungu Comfort Zone Deliberately Dhiki Difficulty Dunia Imekata Tamaa Faith God God Almighty Grace Imani Key Life Maisha Makusudi Matatizo Mungu Mwenyezi Mungu Neema Nguvu Obstacles Peace Of God Power Problems Ufunguo Uwezo Vikwazo Wakati Wa Raha World Has Given Up

Katika dunia ya leo ambapo mamilioni ya watu hutegemea utandawazi kupata pesa, kuwa na imani kwamba kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua au mtu mwenye nia mbaya na wewe ni kikwazo kikubwa cha maendeleo kwa sababu, karibu kila mtu unayekutana naye ni Shetani. Shetani ni mtu yoyote mwenye nia mbaya na wewe. Hivyo, kama uliwahi kuambiwa kwamba kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua ni kitu kibaya futa imani hiyo. Utaachaje kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua wakati kila siku unamwomba Mungu akusaidie, na Mungu hutenda kazi zake pale tunapojisahau? La sivyo hutapata pesa unayotamani kupata katika maisha yako, na kamwe hutawaamini watu. Zaka huondoa laana ya mapato. Toa zaka kununua pepo uliyopewa na Mungu.

~ Enock Maregesi

Enock Maregesi Curse Of Income Development Dunia Faith Globalization God Imani Laana Ya Mapato Life Maendeleo Maisha Malice Mamilioni Ya Watu Millions Of People Money Mtu Usiyemjua Mungu Nia Mbaya Paradise Pepo Pesa Satan Shetani Tithe Unanimous Person Utandawazi World Zaka
  • Classy Quote

    ClassyQuote has been providing 500000+ famous quotes from 40000+ popular authors to our worldwide community.

  • Other Pages

    • About Us
    • Contact Us
    • Privacy Policy
    • Terms of Use
  • Our Products

    • Chrome Extention
    • Microsoft Edge Add-on
  • Follow Us

    • Facebook
    • Instagram
Copyright © 2025 ClassyQuote. All rights reserved.