Classy Quote logo
  • Home
  • Categories
  • Authors
  • Topics
  • Who said

Imani Quotes

Imani quote from classy quote

Amri ya Kristo ilipima imani ya yule kipofu, ikiithibitisha na kuiimarisha. Bila kuchelewa au kusita, kipofu alitii amri ya Mungu: Alikwenda kuosha macho yake katika bwawa la Siloamu na aliona. Wengi wanaweza kuona ni kazi ya kipuuzi kwa mtu ambaye ni kipofu kufanya kazi ndogo kama hiyo ili aone. Lakini kwa vile alitii, kipofu alipona. Baraka huja kupitia utii. Kwa maana nyingine, kipofu alimtii Yesu bila kuona. Lakini matokeo yake, alipata kuona papohapo; ambapo baadaye, hatimaye, alipokea uponyaji halisi wa kiroho.

~ Enock Maregesi

Enock Maregesi Amri Ya Kristo Amri Ya Mungu Blind Bwawa La Siloamu Divine Decree Faith Imani Kipofu The Command Of Christ Utii

Vita ya Shetani na Mungu inatuathiri zaidi sisi wanadamu – na hapo baadaye itamuathiri Shetani pia. Vita hii haiwezi kuisha hadi siku ya mwisho, Yesu Kristo atakaporudi kuwachukua wateule wake. Pambana kwa njia ya maombi hadi siku ya mwisho kwa sababu adui tunayepambana naye hana muda wa kupumzika. Pambana kujiombea na kuwaombea wengine waliohai, na hata wale ambao bado hawajazaliwa, kabla mafuta ya dunia hii hayajalipuka. Usiishi kama adui wa msalaba wa Yesu Kristo, badala yake, ishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Kuishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo ni kupinga majivuno yote ya Shetani kwa upendo uliotukuka wa kujishusha au kujidharirisha, kutokutetereka hata kidogo na tamaa za ulimwengu huu kwa upendo mkubwa wa umaskini, na kutokuyumba wakati wa matatizo kwa sababu wakati wa amani ulijilimbikizia imani.

~ Enock Maregesi

Enock Maregesi Adui Amani Battle Day Of Judgement Elects Enemy Faith Fight Friend God Humans Imani Jesus Christ Love Mafuta Ya Dunia Hii Majivuno Maombi Matatizo Msalaba Wa Yesu Kristo Mungu Needs Oil Of This World Pambana Peace Poverty Prayers Pride Rafiki Satan Shetani Siku Ya Mwisho Tamaa Za Ulimwengu Huu The Cross Of Jesus Christ The Desires Of This World Umaskini Upendo Vita Wanadamu Wateule Yesu Kristo

Pambana na Shetani kwa upanga wa imani ambao ni ukweli kwani ukweli ndiyo utakaokuweka huru.

~ Enock Maregesi

Enock Maregesi Faith Fight Free Huru Imani Pambana Satan Shetani Sword Truth Ukweli Upanga

Kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa raha ni rahisi kuliko kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa shida, na utahitaji imani kuendelea kumwamini wakati wa dhiki. Vipindi vigumu katika maisha yetu hutokea kwa kila mmoja wetu. Kuamini ya kwamba Mungu ana makusudi ya lazima kukuondolea vikwazo katika maisha yako ni vigumu sana wakati mwingine, lakini imani ndicho kitu cha muhimu zaidi unachotakiwa kuwa nacho katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa. Amani ya Mungu, ambayo huzidi hekima na maarifa yote ya kibinadamu, ni kuliamini neno la Mungu kwamba ni la kweli. Bila imani hutaweza kumfurahisha Mungu. Imani ni ufunguo wa nguvu, uwezo na neema ambavyo Mungu ametupangia. Kwa ufupi, Mungu ni mkubwa kuliko wewe na matatizo yako.

~ Enock Maregesi

Enock Maregesi Ability Amani Ya Mungu Comfort Zone Deliberately Dhiki Difficulty Dunia Imekata Tamaa Faith God God Almighty Grace Imani Key Life Maisha Makusudi Matatizo Mungu Mwenyezi Mungu Neema Nguvu Obstacles Peace Of God Power Problems Ufunguo Uwezo Vikwazo Wakati Wa Raha World Has Given Up

Kuna nguzo saba ambazo hazina budi kuzingatiwa kama unataka kuheshimiwa na kuwaheshimu wengine. Kwanza kabisa jitambue: wewe ni nani na unafanya nini hapa duniani. Halafu, kabla ya kusema jambo lolote kwa mtu yoyote fikiria kwanza maana au madhara ya hilo unalotaka kulisema. Kisha jifunze tamaduni mbalimbali na watendee wengine kama vile unavyotaka kutendewa au kama vile wanavyotaka kutendewa. Jifunze kusamehe na kusuluhisha migogoro katika jamii unamoishi huku ukidumisha heshima na utu kwa binadamu wenzako. Jijengee imani kwa watu, punguza upendeleo, fanya kazi kama timu kwani hakuna ‘mimi’ katika umoja ila kuna ‘sisi’, na jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE kwa manufaa ya wote. Kuwa kiongozi katika kila jambo unalofanya na katika kila kitu unachofanya. Jitahidi kufanya jambo au kitu kwa usahihi kwa kadiri utakavyoweza.

~ Enock Maregesi

Enock Maregesi Accuracy All Binadamu Conflicts Cultures Faith Favouritism Heshima Human Humanity I Imani Jamii Jitambue Kiongozi Know Yourself Kuheshimiwa Leader Migogoro Mimi Respect Sisi Society Tamaduni Team Timu To Be Respected Umoja Unity Upendeleo Usahihi Utu We Wote

Kilio kikuu cha Yesu, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?”, yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”, na “Imekwisha”, vilitabiriwa katika Zaburi 22 ili watu waliompinga Kristo waamini kama Yesu alikuwa Masihi. Zaburi 22 ulikuwa wimbo maarufu katika kipindi cha karne ya kwanza, kipindi ambacho Yesu alizaliwa na kufa, uliotungwa na mfalme Daudi, ulioitwa ‘zaburi ya mateso na matumaini ya mwadilifu’. Kwa hiyo Yesu aliposema maneno hayo yaliwaingia watu akilini, na kuanzia hapo imani hasa ya Ukristo ikachukua kasi hadi leo hii. Zaburi 22 inaanza na “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” na inaisha na “Imekwisha”, miongoni mwa maneno saba aliyoyasema Yesu pale msalabani Golgotha. Kwa hiyo, Zaburi 22 ni utabiri wa kifo cha Yesu.

~ Enock Maregesi

Enock Maregesi Christ Christianity Cross Eloi Eloi Lama Sabakthani Faith First Century Golgotha Imani Imekwisha It S Finished Jesus Jesus Death Karne Ya Kwanza Kifo Cha Yesu King David Kristo Maneno Saba Masihi Messiah Mfalme Daudi Msalabani Mungu Wangu My God Psalm 22 Seven Words Song Ukristo Wimbo Yesu Zaburi 22

Katika dunia ya leo ambapo mamilioni ya watu hutegemea utandawazi kupata pesa, kuwa na imani kwamba kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua au mtu mwenye nia mbaya na wewe ni kikwazo kikubwa cha maendeleo kwa sababu, karibu kila mtu unayekutana naye ni Shetani. Shetani ni mtu yoyote mwenye nia mbaya na wewe. Hivyo, kama uliwahi kuambiwa kwamba kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua ni kitu kibaya futa imani hiyo. Utaachaje kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua wakati kila siku unamwomba Mungu akusaidie, na Mungu hutenda kazi zake pale tunapojisahau? La sivyo hutapata pesa unayotamani kupata katika maisha yako, na kamwe hutawaamini watu. Zaka huondoa laana ya mapato. Toa zaka kununua pepo uliyopewa na Mungu.

~ Enock Maregesi

Enock Maregesi Curse Of Income Development Dunia Faith Globalization God Imani Laana Ya Mapato Life Maendeleo Maisha Malice Mamilioni Ya Watu Millions Of People Money Mtu Usiyemjua Mungu Nia Mbaya Paradise Pepo Pesa Satan Shetani Tithe Unanimous Person Utandawazi World Zaka
  • Classy Quote

    ClassyQuote has been providing 500000+ famous quotes from 40000+ popular authors to our worldwide community.

  • Other Pages

    • About Us
    • Contact Us
    • Privacy Policy
    • Terms of Use
  • Our Products

    • Chrome Extention
    • Microsoft Edge Add-on
  • Follow Us

    • Facebook
    • Instagram
Copyright © 2025 ClassyQuote. All rights reserved.