Classy Quote logo
  • Home
  • Categories
  • Authors
  • Topics
  • Who said

Matatizo Quotes

Matatizo quote from classy quote

Vita ya Shetani na Mungu inatuathiri zaidi sisi wanadamu – na hapo baadaye itamuathiri Shetani pia. Vita hii haiwezi kuisha hadi siku ya mwisho, Yesu Kristo atakaporudi kuwachukua wateule wake. Pambana kwa njia ya maombi hadi siku ya mwisho kwa sababu adui tunayepambana naye hana muda wa kupumzika. Pambana kujiombea na kuwaombea wengine waliohai, na hata wale ambao bado hawajazaliwa, kabla mafuta ya dunia hii hayajalipuka. Usiishi kama adui wa msalaba wa Yesu Kristo, badala yake, ishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Kuishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo ni kupinga majivuno yote ya Shetani kwa upendo uliotukuka wa kujishusha au kujidharirisha, kutokutetereka hata kidogo na tamaa za ulimwengu huu kwa upendo mkubwa wa umaskini, na kutokuyumba wakati wa matatizo kwa sababu wakati wa amani ulijilimbikizia imani.

~ Enock Maregesi

Enock Maregesi Adui Amani Battle Day Of Judgement Elects Enemy Faith Fight Friend God Humans Imani Jesus Christ Love Mafuta Ya Dunia Hii Majivuno Maombi Matatizo Msalaba Wa Yesu Kristo Mungu Needs Oil Of This World Pambana Peace Poverty Prayers Pride Rafiki Satan Shetani Siku Ya Mwisho Tamaa Za Ulimwengu Huu The Cross Of Jesus Christ The Desires Of This World Umaskini Upendo Vita Wanadamu Wateule Yesu Kristo

Kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa raha ni rahisi kuliko kumwamini Mwenyezi Mungu wakati wa shida, na utahitaji imani kuendelea kumwamini wakati wa dhiki. Vipindi vigumu katika maisha yetu hutokea kwa kila mmoja wetu. Kuamini ya kwamba Mungu ana makusudi ya lazima kukuondolea vikwazo katika maisha yako ni vigumu sana wakati mwingine, lakini imani ndicho kitu cha muhimu zaidi unachotakiwa kuwa nacho katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa. Amani ya Mungu, ambayo huzidi hekima na maarifa yote ya kibinadamu, ni kuliamini neno la Mungu kwamba ni la kweli. Bila imani hutaweza kumfurahisha Mungu. Imani ni ufunguo wa nguvu, uwezo na neema ambavyo Mungu ametupangia. Kwa ufupi, Mungu ni mkubwa kuliko wewe na matatizo yako.

~ Enock Maregesi

Enock Maregesi Ability Amani Ya Mungu Comfort Zone Deliberately Dhiki Difficulty Dunia Imekata Tamaa Faith God God Almighty Grace Imani Key Life Maisha Makusudi Matatizo Mungu Mwenyezi Mungu Neema Nguvu Obstacles Peace Of God Power Problems Ufunguo Uwezo Vikwazo Wakati Wa Raha World Has Given Up
  • Classy Quote

    ClassyQuote has been providing 500000+ famous quotes from 40000+ popular authors to our worldwide community.

  • Other Pages

    • About Us
    • Contact Us
    • Privacy Policy
    • Terms of Use
  • Our Products

    • Chrome Extention
    • Microsoft Edge Add-on
  • Follow Us

    • Facebook
    • Instagram
Copyright © 2025 ClassyQuote. All rights reserved.